Kiongozi wa Uwekezaji wa Ardhi Tanzania

Tunalinda Na Kukuza Utajiri Wako Kwa Ardhi

Byteq Plots Company Ltd ni kampuni ya daraja la juu inayomiliki, kupima na kuendeleza miradi ya viwanja vyenye hati miliki nchini kote.

Sisi ni Akina Nani?

Kuhakikisha Kila Hatua ya Uwekezaji Wako Inakuwa Salama na Yenye Faida

Tangu kuanzishwa kwetu, Byteq Plots Company Ltd imesimama kama daraja imara la uaminifu kati ya mwekezaji na ardhi halali. Tunaelewa kuwa ununuzi wa ardhi sio tu matumizi ya pesa, bali ni msingi wa urithi na maendeleo ya kizazi chako.

Tukiwa na makao makuu yetu jijini Dar es Salaam, tunajivunia timu ya wataalamu waliobobea katika sheria za ardhi, uratibu wa ramani, na usimamizi wa mali za kiwanja ambao wanahakikisha unapata hati yako bila ukiritimba.

Viwanja Vilivyopimwa Tayari
Ulipaji kwa Awamu
Hati Miliki Haraka
Usimamizi wa Diaspora

"Umiliki wa ardhi iliyopimwa na yenye nyaraka halali ndio siri pekee ya utajiri usiotikisika."

Byteq Plots Co. Ltd

We Map Your Future

5,000+

Hekari Zilizopimwa

3,500+

Wateja Waliopo

100%

Hati Miliki Zilizokabidhiwa

Dira Yetu (Vision)

Kuwa taasisi nambari moja inayoaminika Afrika Mashariki katika kurahisisha umiliki wa ardhi salama na ujenzi wa makazi ya kisasa kupitia teknolojia na mifumo ya malipo yenye tija.

Dhima Yetu (Mission)

Kutokomeza migogoro ya ardhi kwa kuwapatia wateja wetu viwanja vilivyopimwa kwa vipimo vya kisasa, vyenye miundombinu bora na hati miliki halali za kisheria kwa uwazi mkubwa.

Misingi ya Kampuni (Core Values)

Nguzo kuu tatu zinazotofautisha huduma zetu na soko la kawaida.

01.

Uaminifu wa Kisheria

Kila mradi wetu unapitia taratibu zote za serikali na wizara ya ardhi. Hatuzi viwanja vyenye migogoro.

02.

Ubunifu na Miundombinu

Tunauza viwanja vilivyopangwa kimkakati vikiwa na barabara, nishati ya umeme, na maji karibu.

03.

Uwezeshaji wa Kifedha

Mifumo yetu ya malipo ya kidijitali na kidogo kidogo (awamu) inampa nafasi kila mtu kumiliki ardhi.